Dieser Beitrag ist ein Kommentar zu "Christina Higgins 2009. English as a Local Language: Post-colonial Identities and Multilingual Practices. " von Lusekelo, Amani
<1>
Mpendwa Amani,
Nashukuru sana kwa maoni yako juu ya kitabu changu. Nakubaliana sana na wewe juu ya dhamira ya ubepari ndani ya muktadha wa mashindano ya urembo. Lakini sikutafiti mashindano yanayotokea bara -- utafiti huo ni wa Sabrina
Billings (sitaki kuonekana kama nilifanya utafiti huo -
nimesoma tasnifu yake ambayo ni nzuri sana). Billings amechapisha utafiti wake hivi karibuni katika Language in Society (2009).
<2>
Uliandika kidogo juu ya tafsiri nyingine katika kitabu. Hivyo, ningependa kueleza wazi kidogo juu ya tafsiri nilizotumia. Watanzania wanne walinisaidia kutafsiri maneno (hasa kwa nyimbo za Bongo Flava).
Ingawa mimi nilisoma Kiswahili mpaka kiwango cha juu kwenye Chuo Kikuu hapa Marekani, nilishindwa kuelewa maana ya maneno mengi ya mashairi ya nyimbo hizi. Zaidi ya hayo, naona kutafsiri inaleta matatizo mara nyingi (hata kwa Kiingereza kwenda lugha nyingine) kwa sababu ya njia kadhaa za kuelewa na kutumia maana ya lugha. Kama wengi wanavyojua, lugha ya vijana ina maana tofauti kabisa ambayo watu wazima wengi hawajui vizuri -- au hata watu wanaotoka mahali tofauti (k.m., mkoa tofauti au hata kata) wasiyojua. Nilitegemea sana maoni ya vijana ili kupata maana yao (k.m.,"amepunch mpenzi") - tafsiri hiyo si yangu.
<3>
Kweli, nilivutiwa sana na tafsiri na maoni tofauti nilizopata kutoka Watanzania kuhusu maneno mengine, na mada hii ndiyo mada kuu ya kitabu changu. "Gwan" ni neno lingine ambalo maana yake inategemea SANA maoni ya watu. Kutoka upande wa isimu, "gwan" ni neno la mkopo kutoka Jamaica na maana yake ni ‘going on’ au ‘go away’ (na ragga ndiyo muziki inayoathiri Bongo Flava). Lakini miongoni mwa vijana wa Dar es Salaam, "gwan" inaweza kumaanisha kitu tofauti kama "cute" kama ulivyoandika. Mi naona matumizi ya gwan yameathiriwa sana na Kiingereza cha waimbaji wa hip hop Marekani na duniani. Katika lugha ya hip hop (na African American English), kusema ‘She got it goin on’ ina maana ileile na ‘cute.’ Naona si lazima kutia maana moja rasmi au asili rasmi kwa maneno kama hayo kwa sababu yanabadili mara nyingi, na yanatumika tofauti na vijana na wengine. Mfano mwingine ni 'chap chap'. Naona neno hili ni vigumu sana kwa kuweka kitambulisho cha lugha. Nilitegemea maoni ya Profesa Deo Ngonyani na wengine kupata mawazo, lakini, mwishowe, sikusema kwamba neno hili ndilo Kiingereza ama Kiswahili. Tena, hii ndiyo dhamira moja kubwa ya kitabu -- kwamba huwezi kusema kwa uwazi au bila mashaka yoyote kama maneno mengi ni, au yamekuwa, Kiswahili -- au bado ni Kiingereza (tunaweza kusema kuwa maneno mengine yana asili mbili). Hii ndiyo maana ya 'multivocal hybridity' kwangu.
<4>
Asante sana kwa kusoma kitabu changu na kwa nafasi ya kujadili juu ya lugha za kitanzania.
<5>
Christina Higgins
Assistant Professor
Department of Second Language Studies
University of Hawai‘i at Manoa
cmhiggin@hawaii.edu
License
Recommended citation ¶
Higgins C (2011). Comment to the book review by Amani Lusekelo / Kommentar zur Rezension von Amani Lusekelo / Commentaire à l récension d'Amani Lusekelo 2009. Afrikanistik online, Vol. 2011. (urn:nbn:de:0009-10-29556)
Please provide the exact URL and date of your last visit when citing this article.
Fulltext ¶
- Volltext als PDF ( Size 76.3 kB )
Comments ¶
There are no comments yet.
Do you have any additions or comments?
Submit comment.